Numbers 32:1-6

Makabila Ng’ambo Ya Yordani

(Kumbukumbu 3:12-22)

1 aKabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ng’ombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo. 2 bHivyo walimjia Musa, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia, 3 c“Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni, 4 dnchi ambayo Bwana ameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo. 5 eKama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama milki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”

6Musa akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa?
Copyright information for SwhKC